HEKIMA (SWAHILI/CONGO)

SALA YA SOLOMONO YA KUMWOMBA MUNGU HEKIMA

IMETOLEWA KWA KITABU CHA HEKIMA 9:1-18

Omba hii sala mara mingi kila siku. Ipatie watu wengi pia waombe Mungu wapate hekima. Sala zingine zapatikana kwa website hii: www.avemaria832.simplesite.com  Tangaza hii kwa watu wote ukitumia facebook etc.

  1. Mungu wa mababu na Bwana wa huruma, uliyeumba  ulimwengu kwa neno lako,
  2.  na kumtunga mwanadamu kwa hekima yako, ili avitawale viumbe vilivyo anzishwa na wewe, auongoze ulimwengu kwa utakatifu na haki,
  3. atawale kwa unyofu wa moyo;
  4.  Unipe hekima iketiyo kitini mwako, usinitenge mbali na watoto wako.
  5.  Kwa maana mimi ndimi mtumishi wako,  mwana wa mjakazi wako, mtu mzaifu mwenye maisha mafupi, mjinga kwa habari za haki na sheria.
  6.  Kama mtu fulani angekuwa mtimilifu kati ya wanadamu, lakini angekosa hekima itokayo kwako,  huyu angestahili kuhesabiwa kama si kitu.
  7.  Ulinichagua mimi niwe mfalme wa taifa lako, mwamuzi wa waana wa kiume wako na mabinti yako.
  8.  Ukaniagiza nijenge hekalu juu ya mlima wako mtakatifu, na altare mjini unamokaa,  kwa mfano wa hema takatifu uliyo weka tayari tangu mwanzo.
  9.  Kwako iko hekima ijuayo kazi yako iliyokuwapo ulipoumba ulimwengu.  Nayo hujua yapendezayo macho yako, yaliyo maadilifu kadiri ya amri zako.
  10.  Uitume kutoka kiti chako kitukufu iwe msaidizi katika shuruli zangu, nitambue yakupendezayo.
  11. Kwa maana hekima yajua yote na kuyafahamu, nayo itaniongoza kwa utaratibu katika vitendo vyangu; itanikinga kwa nuru yake nyangavu.
  12.  Ndipo hapo kazi zangu zitapendeza, nitalitawala taifa lako kwa usawa, nitakuwa nimekistahili kiti cha baba yangu.
  13.  Ni nani awezaye kujua nia zake Mungu? Ni nani awezaye kuwaza mapenzi yake Bwana?
  14.  Kwani mawazo ya wanadamu yanasita, na fikara zetu zinabadilika.
  15.  Kwa maana mwili utakao oza huitia roho uzito, na hema hiyo ya udongo huelemeza akili yenye shuruli nyingi.
  16.  Kwa shida tuyafahamu yaliyo duniani, na kwa ugumu tuyapata yaliyo mikononi mwetu; lakini ni nani aliyevumbua  yaliyo mbinguni?
  17. Ni nani aliyepata kujua nia zako,  isipokuwa Wewe umetoa hekima, na kutuma roho yako takatifu kutoka juu?
  18.  Ndivyo zilivyonyoshwa njia zao walio duniani, ndivyo wanadamu walivyofundishwa yanayokupendeza, na kuokolewa na Hekima.